Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Nimesikitishwa na tukio la kuuawa Askari wa wanyamapori Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro wakiwa katika harakati za kumtia nguvuni Jangili.
— Lazaro Nyalandu (@LazaroNyalandu) January 22, 2015
Kuongea sio kueleweka,labda watasikia tu ukumbuke ‘kuongea’nako ni kipaji,Unaweza kutumia nguvu nyingi kuongea na usieleweke/usisikilizwe — Mwasiti Almas (@mwasitiJ) January 22, 2015
Azam: Azam FC imerejea salaama Dar es salaam jana usiku ikitokea Kanda ya Ziwa ambako Ilikuwa na mechi mbili za ligi kuu dhidi ya Stand United pale Shinyanga na Kagera Sugar pale Mwanza. Timu imeingia kambini moja kwa moja na leo jioni mazoezi yanaendelea ili kuikabili Simba Sports hapo tarehe 25 January katika uwanja wa Taifa
Blog
BBC: Mtandao wa kijamii wa WhatsApp unawabana watu wanaotumia huduma hio kupitia programu bandia na ambayo haijaidhinishwa ya Android kwa muda wa saa 24.
WhatsApp ambayo inamilikiwa na Facebook, ilisema kuwa imechukua hatua dhidi ya watumiaji wa huduma ya WhatsApp Plus kwa sababu ya wasiwasi kwamba programu hiiyo huenda iksababisha kuvuja kwa taarifa za siri za watumiaji wa WhatsApp.
Programu hio bandia na isio rasmi ya Android inawezesha watumiaji wa WhatsApp Plus kupamba mawasiliano yao wanavyotaka.
Wataalamu wanasema kwamba watumiaji wa Android wanapaswa kuwa makini na kutahadhari kuhusu wanavyodownload programu flani au ‘Apps’.
Mtandao wa WhatsApp ulisema hivi karibuni kwamba ina watumiaji milioni 700 wanaotuma ujumbe bilioni 30 kila siku. Kwa sasa inatoza dola 0.99 kwa watumiaji wake wanaotumia huduma ya WhatsApp Plus kila mwaka.
”Lengo letu ni kuhakikisha kwamba huduma ya WhatsApp ni ya kasi kwa wanaoitumia, hilo ndio jambo muhimu sana kwetu,” alisema msemaji wa kampuni hio.
”Watu wengine wamebuni progarmu ambazo bado hazijaidhinishwa na sasa wanazitumia na WhatsApp , kitu ambacho kinaweza kusababisha kupotea kwa ujumbe au baadhi ya taarifa kuvujishwa. ”
”Bila shaka jambo hili linakwenda kinyume na malengo yetu ya kutoa huduma kwa wateja wetu. Kuanzia leo tutaanza kuchukua hatua kali dhidi ya wanaotumia programu ambazo hazijaithinishwa ili kuweza kutumia programu zetu na pia kuwatahadharisha wanaozitumia programu hizo”.
Kulingana na moja ya maduka ya kuuza programu za kwenye mitandao, programu ya WhatsApp Plus yenyewe ilikuwa imekuwa dowloaded mara milioni 35.
Michuzi
Nkamia alaani vikali maneno ya kibaguzi kwa wachezaji, aitaka TFF ichukue hatua
WIZARA ya Habari Utamaduni na Michezo imeliagiza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutoa adhabu kwa timu ya Ruvu Shooting kutokana na kitendo cha ubaguzi kilichofanywa na wachezaji wa timu hiyo dhidi ya mshambuliaji wa Yanga kutoka nchini Rwanda, Hamis Tambwe.
Akizungumza na Ripota wa Globu ya Jamii, Naibu Waziri wa Habari, Juma Nkamia amesema kuwa TFF isikae kimya kutokana na matamshi ya udhalilishaji juu ya Tambwe na kuiagiza TFF kuchukua hatua za kinidhamu haraka iwapo itathidibitika mshambuliaji huyo alitolewa maneno hayo ya udhalilishaji ili iwe fundisho kwa wengine.
“Hakuna nchi yoyote duniani inayopenda vitendo vya ubaguzi, kitendo ambacho upendi kufanyiwa usimfanyie mwenzie, nimesikia malalamiko ya Tambwe kama ni kweli Ruvu Shooting wamemuita mkimbiza wajue sio kitu kizuri tena wale ni jeshi, nadhani wanajua madhara ya vita.
“Wenzetu Burundi hawakupenda kuingia vitani, hakuna nchi yoyote inayopenda kuwa vitani, vita ni mbaya hata hapa inaweza kutokea, ni jambo la kumshukuru Mungu mpaka leo mna amani, uwezi kujua mtu unayemwambia ameumia kiasi gani na hiyo vita ni ndugu wangapi au marafiki wangapi amewapoteza sio kitu kizuri, naiagiza TFF ishugulikie suala hili kwa kuchukua hatua za haraka.”alisisitiza Nkamia.
Saleh Jembe : PLUIJM AENDELEA KULIA NA UPOTEZAJI WA NAFASI KWA KIKOSI CHAKE
Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema angependa kuona kikosi chake kinashusha asilimia ya upotezaji nafasi.
Pluijm amesema bado anakerwa sana na namna timu yake inavyopoteza nafasi licha ya kutengeneza kwa wingi.
“Hauwezi kushinda kama hautumii nafasi unazozipata. Kwa mfumo, lazima utengeneze nafasi halafu uzitumie na hiyo ndiyo maana ya ushindi.
“Tulipoteza nafasi nyingi katika mechi dhidi ya Ruvu Shooting. Tulifanya hivyo pia katika michuano ya Mapinduzi.
Lugha za kigeni marufuku Ofisi Kwetu.. Serikali Ya Somalia!
Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mahmud amepiga marufuku ya matumizi ya lugha za kigeni katika ofisi za Serikali na kusema kuwa lugha pekee ya mawasiliano itakayotumika katika ofisi hizo ni Kisomali.
Rais Hassan amesema lengo la uamuzi ni kuimarisha lugha hiyo.
Spika wa Bunge la Somalia, Muhammad Sheikh Osman Jawari amesema ni jambo muhimu kwa jamii ya wasomali kuelewa umuhimu wa lugha yao.
Mwananchi: Mafuriko yaikumba Mtwara, nyumba 200 zazingirwa na maji, RC atoa saa 24 yaondolewe
Mtwara. Zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika Manispaa ya Mtwara Mikindani kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha hasara kubwa ambayo thamani yake bado haijajulikana.
Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu ametoa saa 24 kwa wataalam kuhakikisha wanayaondoa maji ndani ya makazi ya watu.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Wilaman Ndile amemwambia mkuu huyo wa mkoa alipotembelea maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko hayo kuwa zaidi ya nyumba 200 zimezingirwa na maji katika mitaa mbalimbali ya manispaa hiyo.
Alisema kuwa hakuna mtu aliyeripotiwa kupoteza maisha kutokana na mafuriko hayo lakini kumetokea uharibifu mkubwa wa mali na vyakula.
“Mvua kubwa zilizonyesha jana usiku zimeshababisha mafuriko haya…tatizo kubwa mji wetu hauna mifereji ya kupeleka maji baharini…athari ni kubwa sana,” alisema Ndile.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook