Ilikua ni taarifa ambayo kiukweli hakuna mtu aliyeitegemea kwa sababu kabla ya taarifa hizi za msiba kusambaa haikuwahi kuripotiwa kuugua au kuwa na tatizo lolote marehemu Aisha Madinda.
December 17 mchana ilitoka taarifa ya kukutwa na umauti Dansa maarufu Tanzania Aisha Madinda,mazishi yake yalifanyika December 19 kwenye makaburi ya Kibada Kigamboni.
Watu wengi wamekua na maswali kuhusu ripoti ya Madaktari kutokana na kufariki ghafla,Feysal Madinda mtoto wa kwanza wa marehemu Aisha Madinda ameongea na millardayo.com na kusema>>’Madaktari ripoti waliyotoa ni Presha ndiyo ilisababisha kifo chake’
‘Nachojua mama ana presha lakini sijajua mshtuko huo wa nini maana walichotuambia alipata mshtuko,unajua sisi waislam hatuingilii sana vitu hivyo,tunaamini Mungu anakuwa ashapanga yake,mwaka 2012 ilishawahi kumtokea hali kama hii lakini tukamuwahisha hospitali’.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook
‘