Chama cha TAC kimekubali ombi la walimu la kupunguza muda ambapo walimu wapya wametakiwa kuhudumia Kaskazini Mashariki mwa Kenya, ama sehemu nyingine yoyote yenye changamoto ambapo sheria za TAC zinahitaji mwalimu kuhudumu zaidi ya miaka mitano kabla ya kuomba uhamisho.
Tume ya kukabiliana na ufisadi imemwagiza msimamizi wa Ikulu ya Kenya, Lorence Leyana na Mbunge Othman Kamana ikiwataka kuandikisha taarifa katika ofisi zao kuhusiana na kisa cha Mbunge Alfred Ketere aliyenaswa katika kanda ya video akiwatusi na kuwatishia maisha Maafisa katika kituo cha kupima magari ambapo aliwataja wawili hao.
Chama cha shule za binafsi kimetishia kwenda mahakamani kulalamikia zoezi la kuwachagua wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza, hatua hiyo imeungwa na maofisa wa kituo cha KNUT kilichopo Rift Valley. ambapo walisema wanafunzi wengi waliofaulu mwaka jana wameshindwa kujiunga na shule ya upili.
Chama Cha ODM kesho kitashiriki katika uchaguzi mdogo utakaofanyika March 17,kata ya Kajada wa mgombea wao baada ya kiti hicho kuwa wazi kufuatia kiongozi wake Joseph Ngaiseri kuchaguliwa na Rais kuwa Waziri wa mambo ya usalama wa ndani wa nchi.
Afisa wa APA anadaiwa kuzuiliwa na polisi katika kituo cha Kinang’ob baada ya kuwadhulumu kingono wasichana wawili wenye umri wa miaka 10 na 12 wakiwa nyumbani kwake na inadaiwa afisa huyo wa usalama alifanya hivyo kwa muda wa mwezi mmoja bila majirani kujua lolote.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook