Inaonekana 2015 ni mwaka ambao baadhi ya wasanii wanakuwa na mipango mizuri juu ya kazi zao, sasa good news ninayotaka kukusogezea ni hii ya msanii wa Hiphop, Godzilla kuahidi kutoa audio na video kwa wakati mmoja.
Akiongea na millardayo.com alisema; “Mipango niliyoipanga mwaka 2015 ni kwamba kila baada ya miezi mitatu nitakuwa natoa wimbo lakini utakuwa hautoki hivi hivi kwani nitakuwa natoa audio na video kwa pamoja, zipo nyimbo nyingi nimesharekodi kwa Pancho Latino na Marco Chali pia kuna wimbo nimemshirikisha Marco Chali audio na video, hii ni idea yangu kwasababu unakuta msanii ukitoa audio inakaa kwa muda mrefu kwa hiyo nimeona nikitoa audio na video shabiki ana enjoy zaidi“– Godzilla.
Kwa hiyo kama wewe ni shabiki wa God zilla kaa tayari kwa ujio huo wake mpya 2015
Hapa kuna sauti ya Godzilla akiongea na millardayo.com, isikilize kwa kubonyeza play hapa.
Hautopitwa na story yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook