Kazi yangu ni kuhakikisha hupitwi na chochote ndio maana natumia muda wangu kukusanyia matukio mbalimbali kuanzia Ofisini,Barabarani,Mitaani mpaka kwenye Mitandao kama hii ya leo.
Bunge limepokea, na kukubali Taarifa ya Kamati ya Hesabu za Serikali pamoja na Mapendekezo na maoni yaliyomo
— Zitto Ruyagwa Kabwe (@zittokabwe) January 30, 2015
Facebook
CloudsFM
WASTARA ACHAGULIWA KUWA BALOZI WA KAMPENI YA ‘NISAIDIE MIMI SHILINGI 500 NIPATE ELIMU’
Msanii wa Bongo Movie,Wastara Juma ameteuliwa kuwa balozi wa kampeni YA ‘Nisaidie mimi Shilingi 500 nipate elimu’’ambayo inalenga kuwasaidia watoto wa kike ambao wameshindwa kuendelea na masomo kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa ada ambapo kampeni hiyo itaanzia katika mkoa wa Morogoro.
Instagram
Kassim mganga:ndugu zangu tusiwasahau ndugu zetu walemavu wana mengi na changamoto nyingi mno za kujadili na sisi, tuwawezeshe kwa namna yoyote ile WANAWEZA #IjumaaKareem.
Blog
BBC: Mugabe ateuliwa kuwa mwenyekiti wa AU
Rais mkongwe wa Zimbabwe Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka tisini, sasa ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa muungano wa Afrika-AU.
Wajumbe walimteuwa Mugabe kwa kauli moja katika mkutano wa AU unaoendelea mjini Addis Ababa-Ethiopia.
Uteuzi wa Mugabe kuongoza muungano huo mkubwa ulio na wanachama zaidi ya arubaini, sasa umeingiza doa ndani ya AU, kwani Mugabe hana uhusiano mzuri na mataifa ya Magharibi, hasa baada ya kukaa uongozini tangu Zimbabwe ilipojipatia uhuru mnamo mwaka wa 80.
Saudia yaahirisha viboko vya mwanablogu
Mamlaka nchini Saudi Arabia kwa mara nyengine tena imeahirisha adhabu nyengine ya viboko dhidi ya mwanablogu Raif Badawi.
Hakuna sababu iliotolewa,lakini awamu mbili za kutoa adhabu kama hiyo hapo awali ziliahirishwa kutokana na sababu za kiafya.
Bwana Badawi amepewa hukumu ya viboko 1000 pamoja na kuhudumia kifungo cha miaka 10 jela kwa kutusi Uislamu.
Mwanaharakati wa Saudia ambaye pia ni wakili Suad al Shammary ambaye alifanya kazi na bwana Badawi katika blogi yake ameachiliwa huru.
Alizuiliwa kwa miezi mitatu bila kufunguliwa mashtaka kuhusu matamshi aliotoa katika mtandao wa Twitter ambayo wapinzani wake walisema yanapinga Uislamu.
Aliyekuwa kiongozi wa makaburu aachiliwa
Kiongozi wa zamani wa utawala wa kiimla wa makaburu nchini Afrika Kusini na ambaye alikuwa kinara wa kuongoza kitengo hatari cha kuwatesa watu weusi, Eugene de Kock, amesamehewa, kuhurumiwa na kuondolewa gerezani.
Eugene Alexander de KOCK alikuwa akitumikia hukumu ya mauwaji na mateso kwa wakereketwa wengi wa chama cha ANC, lakini sasa waziri wa haki na sheria Nchini Afrika Kusini, Michael Masutha, amesema kuwa de Kock ameachiwa huru kwa manufaa ya umoja wa kitaifa.
Alikuwa ametubu mbele ya tume ya haki na maridhiano kwamba alikuwa amesababisha zaidi ya vifo vya watu mia moja na pia kuhusika katika vitendo vya kuwatesa watu kinyama na ufisadi, hasa akiwalenga waliokuwa wakipinga utawala wa ubaguzi wa rangi.
Kanali huyo wa zamani wa polisi aliyekuwa na mataji mengi mno alisamehewa kwa mengi ya makosa aliyofanya, lakini akazuiliwa gerezani kwa makosa dhidi ya binadamu kabla ya kufungwa jela maisha.Tarehe ya kuachiwa huru kwake kwa sasa bado ni siri.
Hivi sasa.co.tz
Jeshi la Polisi wilayami Moshi mkoani Kilimanjaro linamshikilia mwalimu mmoja wa shule ya sekondari kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Koka Moita alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 11:45 katika chumba cha darasa la maabara shuleni hapo.
Kamanda Moita alisema mwalimu huyo alimwita mwanafunzi huyo katika chumba hicho na kuanza kumtomasa mwilini na baadaye alimvua nguo kwa nguvu, kisha kumuingilia.
Ameongeza kuwa kutokana na maumivu aliyoyapata alipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Mawenzi kwa matibabu. Kamanda Moita alisema mtuhumiwa huyo anashikiliwa na jeshi la Polisi hivi sasa.
Saleh Jembe
NGASSA ASEMA ANAREJEA YANGA KWA AJILI YA KUAGA TU!
Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Khalfan Ngassa, amesema kuwa amerejea kundini kuitumikia timu hiyo kwa moyo mmoja lakini kubwa zaidi ni kuwa anataka kuwaaga mashabiki wa Jangwani.
Tangu siku kumi zilizopita, Ngassa hakuonekana Jangwani huku Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Kiboroha akisikika akisema wamedokezwa kuwa staa huyo amekwenda Afrika Kusini kufanya majaribio lakini Ngassa mwenyewe amesema alitimkia Tanga kupumzisha akili kutokana na deni la shilingi milioni 45 analodaiwa na benki, ambalo amesusiwa na viongozi wa Yanga walilokubaliana walilipe kwa pamoja.
Ngassa ameliambia gazeti la maarufu la michezo nchini Tanzania la Championi kwamba amefikia maamuzi ya kurejea kwenye timu hiyo baada ya familia yake kuahidi kumsaidia kulipa deni hilo lililotokana na kiungo huyo kusaini Yanga akiwa ana mkataba na Simba.
Ngassa ambaye ameshajiunga na wenzake kambini Bagamoyo kujiandaa na mechi dhidi ya Ndanda FC itakayopigwa keshokutwa Jumapili, amesisitiza kuwa amepanga kujituma zaidi kuhakikisha Yanga inakuwa bingwa na kufanya vizuri kwenye mechi zote.
“Leo (juzi Jumatano) nimeingia kambini huku Bagamoyo nikiendelea na mazoezi kujiandaa na mechi ya ligi kuu dhidi ya Ndanda FC, hiyo ni baada ya familia yangu kuahidi kunisaidia kulipa deni langu la benki.
“Tumefikia hatua hiyo baada ya viongozi (wa Yanga) kukiuka makubaliano na kunisusia kulipa deni hilo, kiukweli akili yangu imerejea katika hali ya kawaida, hivyo ninaahidi kuitumikia timu yangu kwa moyo kwa kufunga na kutengeneza mabao kama njia ya kuwaaga mashabiki wa Yanga kutokana na mkataba wangu kumalizika mwisho wa msimu huu.
“Kikubwa ninataka kuwaonyeshea hao wanaozusha kuwa kiwango changu kinashuka kutokana na starehe na wanawake hao watatu wanaozusha nimewaoa wakati nina mke wangu mmoja wa ndoa,” alisema Ngassa
TAMBWE: BADO HATUJAFIKIA KIWANGO TUNACHOTAKA NA HATUJAKATA TAMAA
Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe amesema licha ya kutofanya vizuri katika kiwango anachotaka yeye na wenzake, wamekuwa wakiendelea kujituma tu.
Tambwe amesema wamekuwa wakijituma kwa juhudi kubwa huku wakiamini mambo yatabadilika kama hawatakata tamaa.
“Unajua ukiendelea kujituma, hata kama hayaendi vizuri baadaye yanaweza kubadilika na ukafanya vizuri.
“Kitu kizuri mimi na wenzangu hatukati tamaa, hata ukija mazoezini utaona watu wanavyojituma na tuna imani siku itafika tuanze kufanya vizuri,” alisema Tambwe.
Mbeyayetu: TRA MBEYA WAWEKWA KITIMOTO NA WAFANYABIASHARA, WASHINDWA KUTOA MAJIBU WAKATAA KULIPA ONGEZEKO LA KODI
WAFANYABIASHARA wa Jiji la Mbeya walifunga maduka yao wakipinga kulipa mabadiliko ya sheria ya kodi ya 2014, ambayo walidai kuwa imeongeza ututiri wa kodi na kuendelea kuwakamua.
Wakizungumza baada ya kukutana katika mkutano wao uliofanyika ndani ya ukumbi wa Mkapa, Jijini hapa, ulioshirikisha watendaji wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) Mkoa wa Mbeya na jeshi la polisi, wafanyabiashara hao walisema kodi hiyo hailipiki na hawako tayari kulipa.
Awali baadhi ya wafanyabiashara walitoa malalamiko yao mbalimbali kuhusu suaala la sheria mpya ya kodi ya mwaka 2014 kuwa inaongeza kero kubwa kwa wafanyabiashara na itasababisha kukwamisha ustawi wao.
Mmoja wa wafanyabiashara hao, Masaga Salum, alisema mabadiliko hayo ya sheria ya kodi hayawatendei haki wafanyabiashara kwa kuwa hawakushirikishwa katika mchakato wa kuandaliwa kwa sheria hiyo.
“Haiwezekani serikali ikawa inatoa misamaha ya kodi kwa wawekezaji wakubwa toka nje ya nchi , huku ikitumia nguvu kubwa ya ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara wadogo wa hapa nchini ambao ndio wapiga kura wanaowaweka madarakani ”
Global Publisher
Mkurugenzi wa ASET Asha Baraka na Mkurugenzi wa Extra Bango Ally Choki, leo wamemaliza tofauti zao za hapo awali katika ofisi za Global Publishers zilizopo Sinza Bamaga Jijini Dar es salaam. Neno moja la ushauri kwa wakurugenzi hawa!!
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook