Kampuni ya Apple ambayo inafahamika kwa bidhaa kama Iphone , Ipad na Ipod imekuwa kampuni ya kwanza ya kibiashara ulimwenguni kuwa na thamani ya dola bilioni 700 baada ya mauzo ya hisa zake .
Mauzo ya hisa za kampuni hii yalipanda kwa asilimia 1.9 na kufikia thamani ya dola 122.02 na kuinyanyua thamni ya kampuni hii kufikia dola za kimarekani bilioni 710 ikiwa ni kampuni ya kwanza kufikia na kupita thamani ya dola bilioni 700.
Mkurugeni Mtendaji wa kampuni hii Tim Cook alithibitisha taarifa hizi akiwa kwenye mkutano wa Teknolojia wa Goldman & Sachs ambapo alisema kuwa kampuni hii imefikia malengo yake na inafanya kazi katika kiwango cha ubora ambacho kimesaidia kuongezeka kwa thamani yake .
Mkurugenzi huyo amesema kuwa moja kati ya vitu ambavyo vimefanya kampuni yake kuwa bora ni jinsi ambvyo imeingia kwenye mfumo wa maisha ya watu ya kila siku kwa kutumia bidhaa zake ambazo kimsingi zinatoa huduma ambayo ni bora .
Cook amesema kuwa mfumo wa uuendeshaji wa simu za Iphone wa Ios umeinia kwenye maisha ya watu na umeingia kwenye vitu muhimu kama burudani , afya na kazi za kawaida za kila siku jambo ambalo limefanya bidhaa za Apple kuwa na nguvu katika soko hususan soko la mawasiliano ya simu za mkoni na teknolojia ya mtandao wa Internet kwa jumla .
Moja kati ya bidhaa za Apple ambazo zinangojwa kwa hamu sokoni kwa sasa ni simu zake za I ambazo zinafahamika kwa Iwatch ambazo zinatarajiwa kuongeza thamani ya kampuni zaidi ya ilivyo sasa .