Miezi 14 imepita tangu itolewe hukumu ya kifungo cha miaka saba kwa waandishi wa habari wawili na mwingine mmoja kufungwa miaka 10 kwa kosa la kuripoti habari za kichochezi wakiwa ndani ya Egypt wakati wa machafuko ya kisiasa, leo kuna taarifa nzuri kuhusu waandishi hao.
Mahakama ya Misri iliagiza kuachiliwa kwa waandishi wa habari wawili wa kituo cha Aljazeera, Baher Mohamed na Mohamed Fahmy waliohukumiwa kwa kosa la kuandika habari za kutetea kundi la Muslim Brotherhood ambacho baadaye kilipigwa marufuku kwenye nchi hiyo.
Mohammed Fahmy na Baher Mohammed wamekaa jela kwa zaidi ya siku 400 kila mmoja na mwenzao raia wa Australia, Peter Greste alirudishwa nyumbani kwao Australia kwa amri ya Rais Fattah el-Sisi, maamuzi ya Jaji wa Mahakama iliyotoa kibali cha kuachiliwa waandishi hao yanawaweka huru mpaka siku ya February 23 kwa ajili ya kusilizwa upya kwa kesi hiyo.
Ndugu na jamaa wa waandishi hao waliokuwa Mahakamani hapo walipokea kwa furaha taarifa za ndugu zao kuachiwa, huku masikio na macho yao wakisubiri hukumu itakatotolewa kwa mara ya pili.
Great breaking news! @MFFahmy11 is out of bail. Waiting for news on Baher’s release. #cdnpoli #FreeAJStaff pic.twitter.com/TuAgYAMDWh
— Mondee Redman (@MondeeRedman) February 13, 2015
My brother @MFFahmy11 has been released from the police station!! I am going on vacation before they arrest him again! Thank you all! #Adel
— Mohamed Fadel Fahmy (@MFFahmy11) February 13, 2015
Waandishi wengi duniani walilaumu kitendo cha kufungwa Wanahabari hawa wakidai kuwa ‘wamefungwa kwa hatia ya kutekeleza majukumu yao’.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook