Mlinzi wa timu ya Liverpool, Kolo Toure amethibitisha kuwa amestaafu kucheza soka la Kimataifa baada ya kuwa na kikosi cha timu ya Taifa Ivory Coast kwa miaka 15, ambapo ameshiriki pia kuisaidia Timu hiyo kutwaa kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 aliweka wazi kuwa mchezo wake wa mwisho kuonekana kwenye dimba la soka la kimataifa ulikuwa wa dhidi ya timu ya Equatorial Guinea.
Kolo anasema anaipenda nchi yake na hasa anachokipenda zaidi maishani mwake ni mchezo wa soka, lakini amesisitiza kuwa huu ni wakati wake wa kusitisha kuendelea kucheza.
“Najisikia vibaya sana kuwafahamisha kuwa ni wakati wangu kuwaaga, lengo langu lilikuwa kushinda katika michuano ya kombe la mataifa ya Africa.. nakubali ulikuwa ni uamuzi mgumu kutangaza“:- Kolo Toure.
Toure amekuwa kiungo muhimu sana katika kuutengeneza ushindi wa timu na taifa lake katika kipindi cha miaka ya 2006, 2010 and 2014 akiwa na kikosi cha timu yake ya taifa katika michuano ya Kombe la Dunia.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook