Waziri mkuu wa India Narendra Modi alinunua suti ya gharama ambayo aliivaa kwenye mapokezi ya Rais Barack Obama alipotembelea India January 2015 ambapo sasa manunuzi ya suti hiyo yamekua ishu nzito kwenye taifa hilo.
Wananchi wanalalamikia gharama za suti hiyo kwamba haziendani na maisha yao huku Wanasiasa Upinzani wakisema hayo ni matumizi mabovu kuwahi kutokea tena kwa kitu kama Suti.
Suti ya Waziri huyo iligharimu zaidi ya dola 16,000 za Kimarekani ambazo ni zaidi ya milioni 29 za Kitanzania ambapo moja ya vilivyofanya suti hii kuchukua gharama kubwa ni upekee wake, ina mistari midogomidogo ambayo ukiiangalia kwa ukaribu ni maandishi yaliyoandikwa jina la Waziri Mkuu huyo.
Waziri Mkuu Ghandi ametangaza kuipiga mnada suti yake hiyo alafu pesa itakayopatikana ichangie maendeleo kwa watu ambapo hata hivyo kuna dalili kwamba itapatikana pesa ndefu manake mpaka usiku wa February 19 2015 watu walikua wanaigombani na kuifikishia thamani ya dola za kimarekani 201,335 ambazo ni zaidi ya milioni 370 za Kitanzania ikiwa ni zaidi ya mara 10 ya pesa aliyoinunulia.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook