Barnaba ni wa kwanza leo kwenye 255, anaizungumzia video ya ‘Siri’ ambayo anasema walianza kwa kusign mkataba na VEVO ambao waliiachia video hiyo kwa mara ya kwanza baada ya maandalizi ya video kuchukua zaidi ya mwezi mmoja mpaka kukamilika.
Msanii huyo anasema Vanessa Mdee amesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha kupata account hiyo ambapo itamsaidia kuusogeza muziki wake kutambulika Kimataifa.
Barnaba amesema kuwa video hiyo ilipangwa kuwa vile ambavyo imetokea ili kuutangaza utamaduni wetu, haikuwa na haja wao kusafiri kwenda nje.
Wiki iliyopita kwenye 255 kulikuwa na review ya album ya ‘Taswira’ ya Mandojo na Domokaya ambapo walitaja pia kiasi cha pesa ambacho walipata kwenye mauzo ya album hiyo, leo Mandojo amesema pesa walizopata ziliwasaidia kujenga nyumba za wazazi wao pamoja na wao kuishi poa.
Makundi mengi yamevunjika, Mandojo amesema wao wamedumu muda mrefu kwa kuwa wameishi karibu kwa muda mrefu kitu kilichofanya wawe kama ndugu na pia kuishi nyumba moja.
Msanii wa Bongofleva Nuru the Light amesema amewasaidia wanawake wengi ambao wameachana na waume zao au wamefiwa na wana idea ya biashara kuwapatia mitaji kwa ajili ya kuanzisha miradi hiyo.
Nuru amesema kuwa mwaka huu amepanga kuwasaidia vijana ambao watakuwa na changamoto ambazo ziko ndani ya uwezo wake kuzitatua.
Isikilize hapa audio ya 255 niliyoirekodi, bonyeza play uisikie yote.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook