Kama ulikuwa mbali na radio yako kwa bahati mbaya ukapitwa na story za kwenye 255 ziko hapa kwa ajili yako, staa wetu TZ Jokate Mwegelo ambaye mwaka jana ni moja ya mastaa ambao milango ya neema ilifunguka upande wao kwa kusaini deal ya kukuza biashara zake amesema mafanikio yalikuwa makubwa kutokana na mapokezi mazuri ya bidhaa zake sokoni.
Jokate alianza kwa kuuza nywele za kike na zenye brand name ya ‘Kidoti’, baadaye akaingia mkataba ambao umeongeza bidhaa nyingine sokoni TZ ikiwemo ndala ambazo zinapatikana kwa bei ambayo amesema haizidi shilingi elfu kumi.
Baada ya watu wengi kuongelea ishu ya Nikki Mbishi kutangaza kuacha muziki ameamua kurudi rasmi na kuachia ngoma yake mpya ambayo itatoka wiki ijayo na baada ya hapo kutakuwa na tour yake ya kimuziki kwenye maeneo mbalimbali TZ.
Nuh Mziwanda ameomba radhi kutokana na picha ambayo aliiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram, watu wakatoa comment ambazo anahisi kwamba walielewa vibaya picha hiyo, Nuh amesema sababu ya kuweka picha hiyo ilikuwa kama kuwatangazia fans wake kwamba kuna video ya wimbo mpya inakuja na picha hiyo ilikuwa ni sehemu ya behind the scene ya video hiyo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook