Story ambazo huwa zinamzungumzia Kanye West mara nyingi zinakuwa za vioja vioja hivi, najua utakumbuka ya kwenye red carpet ambayo aligoma kutabasamu ili apigwe picha.. mara akamwambia msanii Beck kwamba hastahili Tuzo.. mara ikasikika ya kurushiana maneno kati yake na Amber Rose..
Story ya kumuona Kanye West akitoa machozi hii kidogo inaufunua ukurasa mwingine wa rapper huyo, Kanye alikuwa kwenye Interview katika kituo cha BBC Radio 1, kilichomtoa machozi ilikuwa alipomkumbuka rafiki yake aliyefariki, Prof. Louise Wilson aliyekuwa anajihususha na masuala ya mitindo.
“Mara ya mwisho tumekutana kwenye mgahawa ambao napendelea kwenda nikiwa London, mgahawa wa Hakkasan.. ni kama alijua kwamba anakaribia kufariki, akanipa ushauri mzuri wa kunifanya nifanikiwe kwenye maisha.. aliulizia kuhusu mke wangu na mtoto wangu..“– Kanye West.
Wakati akiendelea na interview hiyo machozi yalimtoka, akajifuta halafu akamwambia mtangazaji Zane Lowe ambaye alikuwa akimfanyia Interview hiyo kwamba hakuwahi kutoa machozi akiwa anahojiwa.
Unaweza kuicheki hapa sehemu hiyo.. Bonyeza play.
https://www.youtube.com/watch?v=9XWslQSbzcc
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook