Taarifa ya kwanza kusikika kwenye 255 inahusu taarifa ya msiba wa mke wa msanii Noorah ambaye walifunga ndoa mwaka 2013.
Noorah amesema yeye alikuwa Shinyanga akiugua akapigiwa simu na kaka yake na marehemu kumpa taarifa za msiba huo hivyo yuko njiani kwenda Morogoro ambako ni nyumbani kwa wazazi wa mke wake, msanii huyo amesema kuwa mke wake alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kifua kwa muda mrefu.
Prof. Jay ni mmoja ya wasanii ambao wametangaza kugombea Ubunge mwaka huu, amesema ameamua kugombea Jimbo la Mikumi kwa kuwa hapo ni nyumbani kwao, wazazi wake waliishi hapo kwa muda mrefu japo wao ni watu wenye asili ya Mkoa wa Ruvuma.
Staa huyo wa Hiphop amesema amekuwa akiimba muziki ambao ni siasa hivyo kaona aingie kabisa afanye siasa kwa vitendo.
Kwa upande wake Inspector Haroun amesema kwa sasa hajaamua kugombea Jimbo la Temeke kama ambavyo alitangaza anataka ajipange kwanza mpaka uchaguzi huu upite.
Ripota wa Clouds FM, DJ Askofu ambaye yuko Mkoa wa Ruvuma amesema taratibu za Mazishi zinaendelea nyumbani kwa Marehemu Kapteni Komba nyumbani kwao Kijiji cha Lituhi, Mbinga ambapo watu wengi wanashiriki katika shughuli hizo ikiwemo viongozi wa Serikali wakiongozwa na Rais Kikwete.
Story zote ziko kwenye hii sauti hapa, bonyeza play uisikilize..
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook