Kwetu TZ kuikuta bidhaa kutoka China kwenye duka lolote sio kitu cha kushangaza kiukweli, kuna radio, simu, TV na bidhaa nyingine nyingi sana ambazo tunazinunua na kutumia ambazo zina maandishi ‘Made in China‘.
Kwa Marekani kumbe kuna bidhaa ikiingia kwenye soko lao ikiwa imetengenezwa China ni ishu ambapo inafanya kuwa habari kubwa kwa upande mwingine.
Joshua Slocum ni mmiliki wa kampuni ambayo inatoa huduma za mazishi anasema mfumo wa Marekani kuruhusu watu ambao wamewekeza kwenye huduma kama ya Kampuni yake kuingiza bidhaa toka nje ni kitu ambacho Serikali imeweka utaratibu mgumu sana ili kuzuia biashara hiyo.
Slocum anasema bei ya jeneza moja Marekani ni kama dola 2000 (zaidi ya Mil. 3 na nusu Tshs) wakati jeneza moja toka China ni kama dola 350 tu (sawa na laki 6 Tshs), lakini Serikali imezuia kabisa kuingizwa kwa majeneza toka China, wakati matumizi yake ni yaleyale na hata ubora na kiwango chake pia.
Jamaa anasema Hillenbrand, Matthews International, and Aurora Casket ndio makampuni makubwa yanayouza majeneza Marekani, wanajipangia bei na utaratibu pia wa kufanya biashara yao kitu ambacho kwa watu wa kipato cha chini wanapata wakati mgumu kumudu gharama za majeneza wakipata msiba.
Slocum hapendezwi na utaratibu huo, anasema wote tutakufa haijalishi umezikwa au umechomwa moto.. Jeneza sio kitu kitakachobadili kitu chochote; “We all go back to the earth. I don’t care whether you’re cremated, whether you’re buried in a sealed American casket or a non-sealed casket, there’s no funeral product on earth that will make you any less dead“– Joshua Slocum.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook