Benki ya NMB imemkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wao mpya, Ineke Bussemaker ambaye anachukua nafasi ya Mark Wiessing ambaye amepangiwa kituo kingine cha Kazi ndani ya Benki ya Rabobank iliyopo Brazil.
Wiessing ataanza rasmi majukumu yake Brazil mwezi wa tano mwaka huu.
Ineke Bussemaker anakuja NMB akitokea Uholanzi ambako alikuwa Mtendaji Mkuu katika Kitengo cha Malipo katika Benki ya Rabobank hivyo ni mtu mwenye uzoefu wa juu wa masuala ya kibenki na biashara ya kimtandao, utaalamu ambao utaisaidia benki ya NMB kukua zaidi.
Kabla ya RaboBank, Ineke alishika nyadhifa mbalimbali za juu katika banki za Citibank, ABN Amro Bank ya uholanzi, Uingereza na Denmark.
Mark Wiessing anaiacha NMB ikiwa imekuwa kwa kasi kwa miaka minne ya uongozi wake, ambapo NMB ina matawi zaidi ya170 na ATM zaidi ya 600 nchi nzima, huku ikiwa na wateja zaidi ya milioni mbili.