Hii ni moja ya story iliyopata Headline kubwa Kenya, inahusu mapacha watatu waliopata alama sawa katika mtihani wa kitaifa wa kidato cha nne KCSE kwenye matokeo yaliyotangazwa Jumanne wiki hii.
Mapacha hao Abenego Bingi, Meshak Barongo na Shadrack Isangoma walipata alama ya B- ambazo ni 55, 56 na 57, wamesema wanapenda sana somo la kiswahili ambalo walifanya vizuri kwenye mtihani huo wa kitaifa.
Mama yao Bi Eugene Amoti ambaye ni Mchungaji katika Kanisa la New Light Kisumu, anasema kuwa mapacha hao walikuwa na viwango tofauti vya kufaulu kwa masomo yao, kila wakati walikuwa wakipata alama tofauti.
Walimu wa Shule ya Kisumu Day wamesema wameshangazwa sana matokeo hayo ambayo wanayaona kama baraka kwa shule hiyo.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook