Wiki iliyopita nilikuwekea story kuhusu mastaa wa muziki wa Marekani, Pharell Williams, Robin Thicke na T.I. walikuwa na kesi Mahakamani, shitaka lililokuwa linawahusu mastaa hao ni ishu ya kutuhumiwa kukopi wimbo wa marehemu Marvin Gaye, ambapo watoto wa mwanamuziki huyo walifungua kesi hiyo.
Wimbo ambao wanatuhumiwa kuukopi ni wimbo wa ‘Blurred Lines‘, moja ya hits ambazo zimependwa sana duniani pamoja na kuingizwa kushiriki kwenye Tuzo kadhaa pamoja na kushinda NAACP Image Awards kama wimbo bora wa collabo mwaka 2014.
Wimbo huo unadaiwa kuwa jamaa walikopi mashairi ya wimbo wa ‘Got to Give It Up‘ ambao ulikuwa hit pia ya Marvin Gaye miaka ya 1970.
Wasanii hao wamekutwa na hatia, hukumu ambayo imetolewa ni kulipa dola Mil. 7.3 (zaidi ya Bil. 133 Tshs), hukumu hiyo inawahusu Robin Thicke na Pharrell Williams ambao kwenye hatimiliki wanatambulika kama waandishi na wamiliki wa wimbo huo.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook