Baada ya kucheza mechi zake nne bila ushindi wowote kwa wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga, August 13 2016 ilikuwa ni nafasi yao ya mwisho kuweza kufufua matumaini ya kuwania kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo kwa kucheza dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.
Yanga ambao walikuwa na point moja katika msimamo wa Kundi A lenye timu za Medeama ya Ghana, TP Mazembe ya Congo na MO Bejaia ya Algeria, walikuwa wanatakiwa kuibuka na ushindi wa aina yoyote ili waweze kufufua matumaini, hata hivyo Yanga ambao hawajawahi kupata ushidni wowote katika hatua ya Makundi toka mwaka 1970 walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0.
Goli pekee la Yanga lililofufua matumaini ya safari ya nusu fainali ya michuano ya CAF, lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi anayeichezea timu hiyo Amissi Tambwe dakika ya 4, kwa matokeo hayo Yanga sasa wanatakiwa kuifunga TP Mazembe ugenini na kuomba mchezo wa Medeama na MO Bejaia umalizike kwa sare yoyote ili wafuzu huku Mazembe akiifunga Medeama katika mchezo wao wa tano.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Yanga haijawahi kupata ushindi wowote katika michuano ya Kombe la shirikisho na klabu Bingwa hatua ya Makundi toka mwaka 1970, na ilikuwa imecheza jumla ya mechi 14, sare 6 na imefungwa mechi nane, ushindi wa leo wa Yanga wanakuwa wameandika historia na kuvunja rekodi yao ya michuano ya kimataifa.
ALL GOALS: Simba vs AFC Leopard August 8 2016, Full Time 4-0