Kama ni shabiki wa soka la Bongo na ungependa kujua hatma ya matokeo ya mechi ya nusu fainali ya Kombe la FA iliyochezwa Tanga katika uwanja wa Mkwakwani kati ya Coastal Union dhidi ya Yanga na ilivunjika wakati Yanga wakiwa mbele kwa goli 2-1 hadi dakika 30 za nyongeza.
Uamuzi uliyofanywa na Kamati ya mashindano ya TFF leo April 27 2016 wakizingatia kanuni ya 28(2) ya Kombe la shirikisho kuwa, Yanga inapewa nafasi ya kufuzu hatua ya fainali baada ya mchezo huo uliochezwa April 24 2016 kuvunjika Yanga wakiwa mbele kwa goli 2-1 na mashabiki wa Coastal Union ndio waliosababisha mchezo uvunjike.
Coastal Union kutokana na mashabiki wake kufanya vurugu katika mchezo huo wamepigwa faini ya Tsh 2000,000, wakati refa wa mchezo huo Abdallah Kambuzi amefungiwa mwaka mmoja na mwamuzi msaidizi namba mbili Charles Simon ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi hiyo ni kwa mujibu wa kanuni 38(1) ya Ligi Kuu.
CHANZO: SALEHJEMBE
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE
ALL GOALS: Yanga vs Al Ahly (Full Time 1-1) April 9 2016 CAF
https://youtu.be/VSM0_i0-DY0