Mchana wa leo November 28 2016 chama cha soka nchini England FA walitangaza kuliona tukio la Jose Mourinho kupiga chupa ya maji kwa hasira wakati wa mchezo kati ya Man United dhidi ya West Ham United uliomalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1.
FA walisema wanasubiri kwanza ripoti ya refa wa mchezo ule Jon Moss ambaye alimuamuru Jose Mourinho kutoka katika benchi kufuatia tukio la kupiga chupa kwa hasira dakika ya 27 ya mchezo, baada ya kuona Paul Pogba anaoneshwa kadi ya njano kwa kudaiwa kujiangusha.
Kama utakuwa unakumbuka Jose Mourinho hilo litakuwa kosa la pili kulifanya ndani ya mwezi mmoja, baada ya October 29 kutolewa katika benchi katika mchezo dhidi ya Burnley na baadae FA ikampiga faini ya pound 8,000 na kufungiwa mechi moja kukaa katika benchi.
Jose Mourinho pia alipigwa faini ya pound 50,000 wakati wa mchezo dhidi ya Liverpool October 17 2016 baada ya kuadhibiwa kosa la kumtolea maneno machafu refa Anthony Taylor.
FA wameona kitendo cha kocha wa Man United Jose Mourinho kupiga chupa kwa hasira, lakini wanasubiri ripoti ya refa kabla ya kufanya maamuzi. pic.twitter.com/YaipuwaqU0
— millard ayo (@millardayo) November 28, 2016
ALL GOALS: Simba vs Toto Africans October 23 2016, Full Time 3-0