Tukio la ajali DAR, hii imetokea leo March 27 2015 eneo la Ilala karibu na Machinga Complex.. Inahusisha treni na lori la mizigo.
Askari wa Shirika la Reli, ASP Mohamed Abdallah ambaye alikuwepo eneo hilo muda mfupi baada ya ajali hiyo kutokea amesema ajali imetokana na uzembe wa dereva wa lori ambaye alitaka kuvuka reli wakati kukiwa na ishara iliyoonesha treni hiyo inavuka.
Askari huyo amesema watu wawili wamejeruhiwa katika ajali hiyo na kupelekwa Hospitali ya Amana kwa ajili ya matibabu.
Mashuhuda wanasema wamemuona dereva wa lori hilo akikimbia huku anachechemea baada ya ajali hiyo kutokea.
Lori hilo lilitokea njia ya Chang’ombe kuelekea Ilala, treni ilitokea upande wa Buguruni kuelekea Stesheni.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook