Baada ya wabunge saba wa kutoka kambi ya upinzani bungeni kusimamishwa kwa makosa mbalimbali na kuchukua vichwa vya habari toka usiku wa mei 30 2016. Wabunge waliosimamishwa kuingia bungeni ni Easther Bulaya, Tundu Lissu,Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema na John Heche.
Sasa Chama cha ACT Wazalendo kimepeleka barua kwa vyama vya upinzani ambavyo wabunge wake wamepatwa na adhabu hiyo ya bunge kuungana siku ya jumapili katika kuwapokea wabunge hao ambao waliosimamishwa kwa muda kutohudhuria shughuli za bunge.
Akizungumza na Ayo TV msemaji wa ACT Wazalendo Abdallah Khamisi amesema….’siku ya jumapili tutakuwa na maandamano ya kumpokea kiongozi wetu na mbunge wetu pekee bungeni kwa maandamano Dar es salaam na katibu mkuu amepeleka barua kwa vyama vingine kushiriki katika mapokezi hayo-Abdallah Hamis
ULIIKOSA HII YA LHRC WALIVYOGUSWA NA KILICHOWAPATA ZITTO KABWE NA WENZAKE ITAZAME HII VIDEO HAPA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE