March 22 2016 Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alifanya mabadiliko ya baadhi ya wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge, huku akiwaondoa wenyeviti na makamu wenyeviti watano katika kamati walizokuwa wakiziongoza baada ya kuwepo kwa tuhuma nzito za rushwa zilizohusisha kamati hizo.
Leo March 23 2016 Chama cha ACT Wazalendo kimetoa msimamo wake juu ya maamuzi yaliyofanywa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwahamisha kamati Wenyeviti, Makamu wenyeviti na Wajumbe wa baadhi ya kamati za kudumu za Bunge uliofanywa jana March 22 2016
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari, Mwenyekiti, Kamati ya Bunge na Serikali za mitaa, ACT Wazalendo, Yeremia Kulwa Maganja amesema …..
>>>’tangu mabunge yaliyopita, kamati za Bunge zimekuwa zikituhumiwa mara kadhaa kujihusisha na vitendo vya kupokea rushwa kutoka kwa mashirika ya Umma, Makampuni na watu binafsi, uamuzi wa kuwahamisha kamati viongozi ni sawa na kuufunika uozo, hili linaendeleza utamaduni mbovu wa siku nyingi hapa nchini wa kuwahamisha au ‘kuwapangia kazi nyingine’ viongozi na watumishi wa umma wanaotuhumiwa kupokea rushwa au kukosa ufanisi‘
>>>’Chama cha ACT Wazalendo kinamtaka Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha mara moja uchunguzi kwa kamati zote zilizotuhumiwa ili ukweli ubainike na hatua zichukuliwe mara moja’
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayokwenye Twitter,FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE