Ujio wa Adele kwenye headlines za muziki umekuwa moja ya matukio makubwa kwenye kurasa za burudani kwa mwaka huu wa 2015. Baada ya ukimya wa miaka minne, Adele alirudi kuchukua nafasi yake kwenye chati za muziki na ujio wa single yake ya kwanza ‘Hello’, single inayopatikana kwenye album yake mpya, 25.
Toka kipindi hicho, wimbo wa Adele umerudiwa na watu wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani, kuanzia mashabiki hadi wasanii wenyewe.
Tumesikia cover za wimbo wake ‘Hello’ ikifanywa na wasanii wa reggae mpaka HipHop na kurudiwa na watu wanaozungumza lugha tofauti lakini hii iliyoimbwa na msanii kutoka Kenya, Dela Maranga kwa lugha ya Kiswahili inaweza kuwa ndio cover bora zaidi kwa mujibu wa mtandao wa Perez Hilton!
Kupitia page yao ya Twitter @PerezHilton mtandao huo umesema cover hiyo ya Kiswahili ina miondoko mizuri zaidi kuliko original version iliyoimbwa na mwenye wimbo, Adele.
>>> “Hii ni INCREDIBLE! RT @Adele’s #Hello kwa Kiswahili inaweza kuwa ndio cover bora zaidi. Isikilize HAPA!” <<< @PerezHilton.
Kupitia website yao, mtandao huo umeandika…
>>> “Dela Maranga ni mwimbaji kutoka Nairobi, Kenya, na Swahili version yake ya 25 classic inaweza kweli ikawa bora zaidi kuliko original version ya wimbo. Sauti yake ni kubwa na yenye nguvu kama ya Adele, lakini pia ina tone nzuri iliyobeba hisia na kufanya mistari ya wimbo ikuguse zaidi – kwa namna ya kipekee.” <<< Wameandika kwenye website yao.
Isikilize cover ya ‘Hello’ kwa Kiswahili hapa chini kwenye hizi dakika tano:
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.