Muongozaji wa video za Bongo Adam Juma leo ameandika ujumbe mzito ambao inawezekana ukawahusu baadhi ya waongozaji wengine wa video za Tanzania .
Kwenye ujumbe wake huo ambao kwenye upande wa picha ameweka camera ameandika maneno haya>>’Watanzania wabishi sana, miaka mitatu tu mtu anaanza kujifanya anajua kumpita mungu’
Anaendelea >>‘kwa style hii hakuna atakae toka i swear to god!!!! Mimi kila siku najifunza ili siku moja nifanye kazi ninayoipenda kwa umakini sio kutengeneza video tu!!!!’
Kingine ameandika>>’Wengine wanaona kushika kamera na kushot ndio mwisho, tunafanya kazi na watu wengine njee tunajifunza sana vitu mkiona nimenyamaza mnaona km f**a vile, ngoja sasa, ota kwanza pata watoto waende shule, jenga nyumba, acha kutumia choo cha baba‘
Adam Juma kamaliza kwa kuandika >>’kama ni shabiki unadomo peleka kwenye sehemu flani amazing za unaempenda kabla kuhujanitest!!! Muda wa majeruhi ukiingia kwenye 18 zangu nakupendezesha alafu tunakuaga leaders’.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.