Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Kwa hii ndege unaambiwa New York mpaka London ni saa tatu tu !!

on

supersonic-jet-nyc

S-512 Supersonic Jet ndio ndege ambayo baada ya kunifikia Ripoti yake ilibidi nishtuke kidogo… eti New York Marekani mpaka London Uingereza ni safari ya saa tatu??

Nimepita mitandaoni ili kuangalia muda wa wastani safari ya toka London mpaka New York kwa kawaida kabisa, nimekuta ni mwendo wa saa saba mpaka nane.. mapinduzi haya hapa, kutoka saa nane mpaka saa tatu !!

staticmap

Spike Aerospace waliitambulisha hii ndege kwa mara ya kwanza 2013, jamaa wameifanyia marekebisho ili iwe salama zaidi kwa wasafiri, ndani ina uwezo wa kubeba watu 18 tu.

FLIGHT

Nimeitafuta hesabu nyingine, umbali wa toka New York mpaka London ni kama Kilometa 5,586 na hiyo ndege inatumia saa tatu.. Safari ya Dar-Kigoma ni kama Kilometa 1,520, kwa maana hiyo ni kwamba S-512 Supersonic Jet itasafiri toka Dar mpaka Kigoma kwa dakika kama 50 hivi.

Ninayo pia kwenye video hapa mtu wangu.

Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments