Usiku wa June 27 ni usiku uliokuwa na burudani nyingi sana hasa kwa zile ambazo uliwahi kuzisikia kipindi cha nyuma kiukweli ni jukwaa lililowakutanisha wakali wengi wa muziki wa zamani wa muziki wa kizazi kipya ambao wengi wao hujapata nafasi ya kuwasikia hivi karibuni.
Miongoni mwa watu ambao niliwaona kwenye stage ambao ni pamoja na Daz Baba,O ten,Mapacha,Man dojo&Domokaya,Jitaman ambao kwa pamoja walipata sapoti kutoka kwa wadogo zao Barakah Da Prince na Chriss Omarya.
Ilikua ni list fulani hivi ambayo iliwafanya watu wengi waliokusanyika ukumbi wa Msamvu Terminal Pub kujawa na hamu mpaka alipokuja kumaliza Afande Sele ambaye alikua mtu wa mwisho kuperfoam ambapo allianza kuuperfoam wimbo wa Elimu Dunia aliyoshirikishwa na Daz Baba.
Baadhi ya picha za show miaka 10 ya Mfalme wa Rhymes iliyokua Morogoro.
Jitta Man kutoka Mwanza nae alikuwepo.
Chigga Son kutoka Planet Fm Morogoro.
Afande Sele na Daz Baba wakiimba Elimu Dunia.
Afande Sele na wadau wa Morogoro
Afande Sele,Man Dojo na Jose wa Morogoro