Waziri wa michezo Misri, Khaled Abdel-Aziz amesema nchi yake imetupilia mbali jitihada za kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2017 ambapo mbali na uamuzi wao wa kujiondoa wameahidi kuiunga mkono Algeria.
Shirikisho la Soka Afrika linatarajia kutoa jina la wenyeji wa michuano hiyo mwezi April ambapo Libya nayo ilikuwa miongoni mwa nchi hizo lakini ilijiondoa kutokana na hali ya kisiasa inayoendelea nchini humo, hata hivyo Waziri huyo hakutoa sababu zilizowafanya wajiondoe kwenye kinyanganyiro hicho japo uamuzi huo umekuja baada ya mjumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA kusema haina maana kwa nchi mbili za Kiarabu kushindania zabuni ya kuandaa mashindano hayo.
Waziri Khaled amesema Misri haitaweza kushindana na Algeria wataunganisha nguvu kushirikiana ili Algeria ishinde nafasi hiyo.
Hali si shwari upande wa Misri kutokana na ishu iliyojitokeza ya vifo vya mashabiki 22 mwezi February wakati Polisi walipokuwa wakipambana na mashabiki kabla ya mchezo kati ya Zamalek na ENPPI, shughuli za soka zimesimama kwa muda usiofahamika.
Bonyeza play ili kuweza kusikiliza taarifa yote niliyokurekodia kwenye kituo cha WBS.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram, na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook