Nchi ya Tanzania imetajwa itakuwa na watu wapatao 299.133 million ifikapo mwaka 2100 wakati ambapo idadi ya watu Duniani ikitarajiwa kufikia 11.2 billion, kwa mujibu wa makadirio ya UN Population Division.
Hadi kufikia mwaka 2100 ambao utakuwa mwisho wa Karne ya 21, Bara la Afrika litaendelea kuongeza idadi ya watu ambapo kwa mujibu wa makadirio hayo mwaka huo Afrika itakuwa na watu zaidi ya 4 billion, ‘39%’ ya watu wote Duniani ikiingiza nchi 9 katika Top 20, lakini ikiwa na nchi 5 katika Top 10 ya nchi zitakazokuwa na watu wengi zaidi Duniani.
Bara la Asia litakuwa na 44% ya watu wote Duniani wakati idadi ya watu Bara la Ulaya ikipungua hadi kufikia 6%, Amerika ya Kaskazini itakuwa na 4%, Latin Amerika 6% na Oceania 1%.
Tanzania itakuwa katika nafasi ya 8 Duniani na itakuwa katika nafasi ya tatu Afrika huku pia ikitarajiwa kuwa kinara kwa watu wengi ukanda wa Afrika Mashariki.
Nigeria itakuwa kinara kutoka Afrika ambapo inakadiriwa itakuwa na watu 752.247 million ikiwa pia katika nafasi ya tatu kidunia nyuma ya India na China.
Top 10 ya nchi zitakazokuwa na watu wengi zaidi duniani mwaka 2100:
VIDEO: Alichokisema Freeman Mbowe baada ya CHADEMA kukosa wabunge katika Bunge la Afrika Mashariki. Bonyeza play kutazama.