2014 inaisha na goodnews kwa East Africa… Majina ya mastaa ambao wamefanya vizuri upande wa Afrika Mashariki 2014 yameongezeka, tumeziona jitihada za mastaa mbalimbali kutoka na kufanya kolabo na wakali wengine kutoka Afrika na pia kurekodi nyimbo na video zao na makampuni makubwa.
Matunda ya jitihada hizo yanaonekana, AFRIMA Awards 2014 zilizokuwa zikifanyika jana December 27 Lagos, Nigeria zimeonyesha dalili njema ambapo Vanessa Mdee ‘Vee Money’ alifanikiwa kuibuka mshindi wa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki, Diamond Platnumz akashinda Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika Mashariki, huku Tuzo ya Wimbo Bora wa Pop ikichukuliwa na msanii Elani kutoka Kenya na Radio na Weasel kutoka Uganda wakipata Tuzo ya Wimbo Bora wa Reggae.
Nakuhakikishia kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook