Video Queen Agness Gerald maarufu kama ‘Masogange’ ambaye ametokea kwenye video kadhaa za muziki wa Bongofleva, leo alifikishwa Mahakamani Kisutu Dar es salaam kufuatia kuitwa Polisi kwa sakata la dawa za kulevya.
Baada ya kushikiliwa na Polisi toka alipokamatwa, Masogange leo amepata dhamana ya shilingi Milioni 10 na hatotakiwa kusafiri nje ya Dar es salaam ambapo kesi yake itakuwepo tena Mahakamani March 22 2017.