August 30, 2018 Waziri wa mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa kikao kazi cha makamanda wa zimamoto na uokoaji nchini kilichofanyika mkoani Dodoma ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa taasisi zinazokwepa kulipa kodi.
“Serikali imekusudia kubadilisha maisha ya Watanzania na kubadilisha utamaduni wa kutolipa kodi na wizi wa mapato ya Serikali ili fedha zinazopatikana zielekezwe kwenye miradi ya maendeleo” –Kangi Lugola
“Nichukue fursa hii kukupongeza Kamishna Jenerali, Makamisha, Maafisa na Askari kwa juhudi kubwa mnazofanya katika kusimamia ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali hasa ukizingatia changamoto zinazowakabili” –Kangi Lugola
“Hongereni sana. Nitumie fursa hii pia kuwataka msimamie mapato yanayopatikana yaingie serikalini badala ya kuingia kwenye akaunti binafsi za watu” –Kangi Lugola
DC Jerry Muro alivyomaliza mgogoro wa miaka 13 wa Kanisa