Kampeni za Vyama vya Siasa bado zinaendelea nchini katika Mikoa mbalimbali na leo September 4, 2020 nakusogezea ahadi alizotoa Mgombea Urais wa Tanzania Bernard Membe akiwa katika moja ya mikutano yake Mkoani Lindi.
“Pindi mkituchagua, tutahakikisha hadi mwaka 2025 asilimia 60 ya watu wote wanaojihusisha na shughuli za kilimo, uvuvi, ufugaji na biashara ndogo zilizosajiliwa wamekuwa na Hifadhi ya Jamii na wananchi wote kuwa na Bima ya Afya” Membe
“Tutasimamia upatikanaji wa maisha stahiki ya uzeeni kwa kuwa na mfumo madhubuti wa Hifadhi ya Jamii ambao utahakikisha kuwa kila Mtanzania anakuwa na Bima ya Afya na Pensheni akifika umri wa kutoweza kufanya kazi” Membe
“Tutahakikisha elimu ya Afya inawafikia Watanzania wote ili wawe na uwezo wa kulinda afya zao na kujiepusha na maradhi yanayoambukiza na yasiyoambukiza, hasa yanayotokana na mfumo wa maisha (life style diseases) na majeraha” Membe
“Tutaunda mfumo wa huduma za afya kwa kuzingatia misingi ya usawa na ushirikishwaji wa jamii katika kufanya maamuzi yanayohusu maswala ya afya,sera bora za huduma za afya,na kuchochea uwajibikaji,ili kupunguza kwa asilimia 30 vifo vya mapema” Membe
“Tutaiboresha bajeti ya huduma za afya mwaka hadi mwaka ili kuboresha elimu ya afya, nguvu kazi, upatikanaji wa dawa na vitendea kazi, teknolojia, miundombinu pamoja na mfumo mzima wa kutoa huduma za afya ambao utatumika nchi nzima” Membe
“Tutaisimamia kikamilifu haki ya kila Mtanzania kuwa na Bima ya Afya yenye kumpa kinga ya matibabu bila kujali hali yake ya kiafya (wakati wa kujiunga na bima)” Membe
INASIKITISHA MATESO ALIYOPEWA MMAREKANI MWEUSI HADI KUFARIKI, POLISI HAWAKOMI