Ndege ya abiria ya Air France Boeing 777 AF463 iliyokuwa ikifanya safari yake kati ya Mauritius na Paris ililazimika kutua ghafla katika uwanja wa ndege wa Mombasa nchini Kenya baada ya kuwepo hofu ya bomu ndani ya ndege hiyo.
Wakati iko angani kuna kitu kilichodhaniwa kuwa bomu kilipatikana ndani ya choo cha ndege hiyo na muhudumu mmoja akachukua hatua ya kumfahamisha Rubani kuhusiana na hicho kifaa ndipo shughuli za kutua kwa dharura zikaanza.
Katika mtandao wake wa kijamii wa Twitter, kamanda mkuu wa polisi Kenya Jenerali Joseph Boinnet, amesema kuwa ndege hiyo iliyokuwa njiani kuelekea Paris Ufaransa ikiwa na abiria 473 na wahudumu 14 na ilitua salama na abiria wote kuokolewa.
Air France B777 Flight 463 on the runway at Moi International Airport, Mombasa Cc @JBoinnet pic.twitter.com/1VfpYR4XHo
— KBCChannel1 (@KBCChannel1) December 20, 2015
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.