Mkurugenzi wa Konvict Muzik na lebo ya KonLive, Akon anajulikana kwa kuwatoa kimuziki wasanii wakubwa Marekani baadhi wakiwa T-Pain na Lady Gaga ambao uwezo wao dunia nzima inashuhudia… lakini ulikuwa unajua kuwa Akon alikataa kumsimamia Drake kipindi hicho rapper huyo anahangaika kutoka kimuziki!? sababu zake?
Akiwa kwenye interview na Montreality online TV ya Marekani, Akon aliulizwa kwa nini aligoma kumsimamia Drake kipindi hicho na je anajutia maamuzi hayo sasahivi? Akon alikuwa na haya yakusema…
>>> “Kweli kipindi hicho nilikataa kumsimamia Drake kwasababu alikuwa tofauti sana na jinsi alivyo sasahivi… kwa mfano wimbo wa ‘The Best I Ever Had’ ulikuwa tofauti sana kipindi kile anaileta demo hiyo kwangu. Nadhani alikuwa bado anatafuta sauti yake na aina ya muziki ambao angependa kuufanya… lakini kwa wakati ule Drake hakuonekana kama biashara nzuri kwangu wala lebo yangu… alikuwa muoga sana na mwenye aibu kubwa, siwezi kusema najutia maamuzi yangu ila kwa kipindi kile sikuona kama angeniletea faida kifedha ila kadri miaka ilivyokwenda confidence ya Drake ilikua sana, hata akiwa on stage unaweza kuona kuwa amekua sana kimuziki, amejifunza kuimiliki audience kwa asilimia mia, he is good”. <<< Akon.
Licha ya Drake kukataliwa na Akon msanii huyo aliendelea na safari yake ya muziki na sasa hivi ni miongoni wa masataa wenye majina makubwa kwenye muziki wa HipHop Marekani akiwa chini ya Cash Money Records ya kwake Birdman na Lil Wayne.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE