Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Mwinyi amechukua fomu ya uteuzi kutoka Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kuweka wazi kuwa dhamira iliyomsukuma kugombea nafasi hiyo ni kuwatumikia Wazanzibari.
“Nimeamua kugombea nafasi hii kwa dhamira moja tu, nayo ni kuwatumikia Wazanzibar, kwahiyo kuweni na matarajio na Inshaallah mwenyezi Mungu akitujalia kwa kushirikiana tutayatimiza” Mwinyi
“Sisi sote tuhakikishae tunahubiri amani na kila mmoja ahakikishe anailinda amani bila ya amani hakuna maendeleo ,bila ya amani hata ibada hatutazifanya tuhakikishe tunailinda amani tuliyonayo” Mwinyi