Mwanaume mmoja nchini India, ameshtakiwa kumuua mke wake na kumuwekea nyoka aina ya ‘cobra amng’ate, amehukumiwa kifungo cha maisha mara mbili.
Sooraj Kumar alikamatwa mwaka jana baada ya mke wake Uthra, kufariki na kukutwa na alama ya kung’atwa na nyoka.
Polisi walianza kufanya uchunguzi baada ya familia yake kutoa shutuma za mauaji na kusema Sooraj alikuwa akiwanyanyasa kwasababu ya mahari.
Jumatatu, Mahakama ilimkuta Sooraj na hatia ya kumuachia cobra atembee kwenye kitanda chao wakati Uthra akiwa amelala.
Polisi wamesema uchunguzi umebaini kuwa bwana Sooraj alikuwa anahusika na majaribio mawili ya mashambulio ya nyoka wote wawili . Aidha wamemkamata pia mwanaume aliyemsaidia kupata nyoka hao – ingawa alisaidia polisi kutoa ushahidi dhidi ya kesi hiyo.
Kwa mujibu wa sheria ya India, Polisi wamemshikilia baada ya kubaini njama walizotumia kufanya uhalifu.
Mahakama imekubali kuwa kesi hii ya nadra inapaswa kupata adhabu mara mbili ya kifungo cha maisha. Hivyo Sooraj amehukumiwa kifungo cha maisha na kutakiwa kulipa dola $6,635.