Mwezi uliopita mahakama ya Misri ilitoa hukumu kwa waandishi watatu wa habari kutoka kituo cha Aljazeera baada ya kukutwa na kosa la kuandika habari za uongo na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela.
Habari njema kutoka nchini humo zinasema Rais wa nchi hiyo Abdul Fattah al-Sisi ametoa misamaha kwa wafungwa 100 wakiwemo waandishi hao.
Waandishi hao Mohammed Fahmy, raia wa Canada, na Baher Mohamed, raia wa Misri ambao hata hivyo walikana tuhuma hizo kuanzia leo watakuwa huru.
Walishtakiwa kwa kosa la kushirikiana na kundi la Muslim Brotherhood la Rais Mohammed Morsi baada yake kuondolewa madarakani na wanajeshi mwaka 2013.
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE