Kwa mara ya kwanza Staa wa Bongofleva Alikiba amefunguka kuhusu Mke wake Amina kuwa na ujauzito katika Interview na Radio Jambo ya Kenya alipokwenda kwa ajili ya kutangaza kinywaji chake cha MOFAYA .
Alikiba amefunguka na kusema hakukutana na Mke wake Amina Mombasa kama Watu wanavyofikiri bali walikutana Nairobi na wakati huo Amina alikua Shabiki yake mkubwa akiwa ni Mwanafunzi wa Chuo cha United States International (USIU).
Alikiba amesema >>>“Katika dini yetu tunaamini ni faida kubwa ya ndoa Mtu kupata ujauzito, baada ya ndoa tu Mke wangu akapata baraka na Mungu akipenda mwakani tutabahatika kupata Mtoto, hatutajua ni Mtoto wa jinsia gani tunasubiria surprise, atakua Mtoto wangu wa nne”
“RAMMY GALIS HAWEZI KUWA KANUMBA” – DIRECTOR JOHN LISTER, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA