Wiz Khalifa na Amber Rose walidumu kwenye uhusiano kwa mwaka mmoja tu tangu wafunge ndoa yao na baadaye wakaachana, kila mmoja alitoa sababu kwamba mwenzake ndio tatizo.
Wiz amesema anajipanga kufungua mashtaka dhidi ya mzazi mwenzake huyo ambaye amedai kuwa amemtelekeza mtoto wao Sebastian kwa kushindwa kumpa matunzo mazuri kama mama.
Wiz amelalamika kuwa mtoto wake amekuwa akilelewa na ndugu zake kwa muda mwingi baada ya mama yake kuwa busy na mambo yake.
Hakuna Stori itakayokupita mtu wangu,niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook