Kipindi cha nyuma Amber Rose na Wiz Khalifa walimake headlines kubwa kuhusu kuachana kwao na kusababisha mada za kila aina katika social networks za Twitter na Instagram. Lakini baada ya yote hayo kupita, Amber siku chache zilizopita alifanya interview na radio station moja jijini Los Angeles na alikua na haya ya kusema kuhusu hali yake sasa na wanaume anaokutana nao >>>
“Wanaume siku hizi wananiogopa, wanaogopa kua na mimi, siku hizi mimi kutongozwa imekua ngumu kidogo sio kama zamani unakuta mtu anakuja anajaribu kuniongelesha na kuniomba namba na vitu kama hivyo… siku hizi haiko hivyo, wanaume wengi sasa hivi wanaishia tuu kuomba selfie na mimi kunisifia nimependeza lakini kutongoza wanaogopa!… Imefika hatua sasa hivi nikivutiwa na mtu inabidi mimi ndo nimuanze bila hivyo…hapana.“
Alipoulizwa kuhusu tattoo ya jina la Wiz Khalifa iliopo mkono wake wa kulia, Amber Rose alisema kwa sasa hana mpango wowote wa kuiondoa tattoo ya jina la Wiz Khalifa;
“Mimi na yeye tuna mtoto, mtoto ambae kila akiiona hii tattoo anafurahi… Labda ije itokee nataka kuolewa na huyo atakaye kua ananioa asipende kuiona hii tattoo mwilini mwangu, labda hapo ndo nitapata sababu ya kuiondoa tattoo ya Wiz Khalifa mwilini mwangu“.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.