Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anaingia uwanjani hii leo kukabiliana na Atletico Madrid huku akifahamu fika kuwa mustakabali wake kama kocha wa klabu hiyo unategemea sana aina ya matokeo ambayo klabu yake itayapata.
Ancelotti aliiongoza Madrid kutwaa mataji manne katika kipindi cha miezi 12 ya mwaka 2014 lakini mwaka huu umekuwa mgumu kwa kikosi chake ambapo timu hiyo imejikuta ikishushwa kwenye kilele cha ligi kuu ya Hispania huku FC Barcelona wakiwa wanaongoza ligi hiyo.
Madrid wanaingia kwenye mchezo wa leo dhidi ya Atletico huku wakiwa wamejawa hofu baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wowote kati ya michezo saba ambayo imezikutanisha timu hizi kwa msimu huu.
Katika michezo ambayo imezikutanisha timu hizi mbili msimu huu kwenye mashindano mbalimbali Real Madrid imepoteza michezo minne huku kukiwa na sare katika michezo mitatu na Real wakiwa hawana ushindi hata mmoja.
Hali inazidi kuwa ngumu kwa Mtaliano huyu pale anapotazama orodha ya majeruhi kwenye kikosi chake ambapo Luka Modric, Karim Benzema na Gareth Bale wote wameumia huku Marcelo akiwa nje ya mchezo huu akitumikia kifungo cha mechi moja baada ya kuonyeshwa kadi za njano mfululizo.
Tetesi ndani ya klabu hii ambayo inatetea ubingwa wake wa ligi ya mabingwa zinasema kuwa kocha mpya atatafutwa msimu ujao huku taarifa nyingine zikidai kuwa Zinedine Zidane anaandaliwa kuchukua nafasi ya Carlo.
millardayo.com ni sehemu yako utakapozipata zote unazozitaka, vichekesho, stori za siasa, muziki, michezo, ovies,nmagazeti,nvideompya na nyingine kubwa…. unawez kujiunga na mimi Facebook, Twitter na Instagram pia zitakufikia zote mtu wangu, jiunge hapa >>>twitter Insta Facebook