Staa wa tennis duniani anayekamata nafasi ya pili kwa ubora Andy Murray amemshinda raia wa Australia Sam Groth na kufika raundi ya tatu ya mashindano ya tenisi ya Australian Open.
Mchezaji huyo aliyeorodheshwa nambari mbili katika mashindano hayo, alimshinda Groth kwa seti 6-0, 6-4, 6-1 katika muda wa saa moja na nusu.
Murray sasa ameingia katika hatua ya 32 bora ambapo atakutana na Mreno Joao Sousa kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka minne.
Kwa upande wa wanawake Johanna Konta alimshinda Zheng Saisai kutoka China kwa seti 6-2 6-3 na kufika raundi ya tatu ya mashindano hayo.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE