Robin Gosens wa Club ya Atalanta ya Italia hivi karibuni alieleza masikitiko yake kwa kugomewa na Cristiano Ronaldo wa Juventus kubadilishana jezi.
Robin (26) ni shabiki na anamtazama Ronaldo kama role model wake lakini 2019 katika robo fainali ya Coppa Italia baada ya kuitoa Juventus kwa ushindi wa 3-0.
Baada ya mchezo alimfuata Ronaldo na kumuomba wabadilishane jezi lakini Ronaldo alikataa kwa kumwambia Hapana huku akiwa hamuangalii hata usoni, Gosens hivi karibuni alieleza kuumizwa na tukio hilo.
“Baada ya mchezo nilijaribu kutimiza ndoto yangu hata sikushangilia na wenzangu nikamfuata Ronaldo kutaka kutimiza ndoto ya kuwa na jezi yake kwa kubadilishana lakini alijibu Hapana hata hakuniangalia usoni”
Sasa baada ya wachezaji wenzake wa Atalanta kusikia hilo kupitia interview aliyoifanya hivi karibuni waliamua kum-surprise kwa kumnunulia jezi ya Juventus ya Cristiano Ronaldo na kumpatia kama zawadi.