Ikiwa homa ya dirisha dogo la usajili inazidi kuchukua headlines Tanzania, vilabu vikiendelea kusaka saini za wachezaji zinaowataka waongeze nguvu vikisoni mwao kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa December 15, nchini Uingereza homa ya dirisha dogo la usajili inazidi kuchukua headlines katika vilabu kadhaa ikiwemo Arsenal.
Kwa kiasi kikubwa klabu ya Arsenal inahusishwa kufanya usajili wa mchezaji au wachezaji wanafasi ya kiungo, Arsenal kwa sasa ambayo inasumbuliwa na wachezaji wake kuwa majeruhi, hivyo inahusishwa kwa karibu kutaka kusajili wachezaji wa nafasi ya kiungo ambao ndio wengi wao majeruhi kikosi mwao.
Kwa sasa Arsenal ina wachezaji watano ambao ni majeruhi Aaron Ramsey, Francis Coquelin, Mikel Arteta, Jack Wilshere na Alex Oxlade-Chamberlain ila inahusishwa kutaka kuwasajili Luiz Gustavo, Christoph Kramer, Lucas Biglia, William Carvalho, Grzegorz Krychowiak, Cheikhou Kouyate, James McCarthy, Ever Banega na mkenya Victor Wanyama anayekipiga katika klabu ya Southampton ya Uingereza miongoni mwa majina hayo usishangae kama jina moja wapo likijiunga na Arsenal mwezi January.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.