Hatua ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka wakili mwandamizi na ofisa wa kituo cha sheria na haki za binadamu Arusha, Shilinde Ngalula kumechukua sura mpya baada ya mawakili Chama cha wanasheria Tanganyika ‘TLS’ Arusha kulaani na kutembea kuelekea makao makuu ya jeshi la polisi Arusha kwa kile wanachokiita ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu unaofanywa na jeshi la polisi dhidi ya wakili mwenzao Shilinde Ngalula na makundi mengine.
Shilinde anadaiwa alikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kwenda kuwasikiliza na kuwatetea watu waliokamatwa na polisi Arusha na akaunganishwa kwenye tuhuma zilizokuwa zikiwakabili watu hao. Rais wa chama cha mawakili kanda ya kaskazini, Modestus Akida amesema……..
>>’matukio kama hayo Arusha yameshatokea mara kadhaa, yale mahusiano kati ya polisi na wakili naona yanaporomoka kwa hiyo tunaenda kwa RPC tumueleze hayo, kosa ambalo asubuhi halikuwepo mchana linakuwepo sasa anaambiwa ni kosa la uhaini lakini usiku aliandika maelezo kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kana kwamba yeye alikuwa amezuiliwa na polisi‘
ULIKOSA HUU UFAFANUZI KUHUSU PIKIPIKI ILIYOPAKIZWA KWENYE BASI LA MWENDOKASI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI