Michuano ya 46 ya Copa America inaanza rasmi usiku wa kuamkia kesho June 15 2019 Saa 9:00 Alfajiri hadi July 7 ambapo mechi zitachezwa katika majiji matano nchini Brazil, Copa America itahusisha jumla ya timu kumi na mbili zikiwemo Japan na Qatar ambao timu wageni waalikwa kushiriki.
Brazil wameahi kuwa wenyeji wa michuano hiyo mara nne na mara zote hizo wameweza kulibakisha Kombe nyumbani, Usiku wa leo wanaanza kibarua cha kutunza rekodi hiyo watakapocheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Bolivia saa 9:30 Alfajiri, Michuano hiyo itachezwa kwenye viwanja 6 katika majiji matano huku fainali ya July 7 ikipigwa katika dimba la Estadio de Maracana jijini Rio de Janeiro.
Timu 12 zinazoshiriki zimepangwa katika makundi matatu yenye timu nne kila moja, ambapo timu mbili za juu kwenye kila kundi zitaingia moja kwa moja kwenye hatua ya mtoano huku timu mbili kwenye nafasi ya tatu lakini zina rekodi nzuri (best loser) zikiungana nazo kwenye hatua ya mtoano.
Brazil watamkosa mshambuliaji Neymar ambaye aliumia kifundo cha mguu kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Qatar, hata hivyo bado wana kikosi kizuri chenye uwezo wa kulibakisha Kombe kwenye ardhi ya nyumbani. Lionel Messi ndiye atatupiwa macho na watu wengi, hii ikiwa ni nafasi yake ya dhahabu kushinda Kombe hilo akiwa na timu ya taifa ya Argentina.
Japokuwa ameshinda kila taji akiwa na club ya Barcelona na mataji binafsi, Messi bado hajashinda kombe lolote akiwa na timu ya taifa (ya wakubwa) na muda ni kama unaelekea kumtupa mkono, Msimu huu Messi atakuwa na shauku ya kuongezea kwenye mataji 14 ambayo Argentina wamewahi kushinda.
Argentina wamepangwa katika kundi B pamoja na Colombia, Paraguay na mabingwa wa Bara la Asia Qatar, Wataanza kampeni yao siku ya Jumapili saa 7:00 Usiku dhidi ya Colombia, Chile wao wataanza michuano dhidi ya Japan siku ya Jumanne saa 8:00 Usiku, michuano hii itaonyeshwa na StarTimes.
EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega