Waandishi watatu wa habari wa Televisheni ya NTV Linus Kaikai, Larry Madowo na Ken Mijungu usiku wa jana wamelazimika kulala kwenye ofisi za kituo hicho cha televisheni kwa kuhofia kukamatwa na polisi kufuatia suala la ‘kuapishwa’ kwa Kiongozi Mkuu wa Upinzani NASA Raila Odinga.
Inaelezwa kuwa askari wasio na sare walikuwa wakizunguka nje ya jengo la kituo hicho kwa lengo la kuwakamata waandishi hao watatu kwa sababu ambazo bado hazikuwa wazi.
Jana Jumatano January 31, 2018 Katibu wa Mambo ya Nje wa Kenya Fred Matiang’i alitangaza kuwa serikali imeanza kuwachukulia hatua wote waliohusika kwa namna yoyote katika zoezi la ‘kuapishwa’ kwa Raila Odinga.
‘Ni kosa kufungisha Ndoa kama Haujasajiliwa’ Jane Barongo