Kamanda wa Keshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Awadh Juma Haji akizungumza na Waandishi wa habari Visiwani Zaznibar ametoa ripoti za matukio mbalimbali yaliyojitokeza Visiwani humo.
Katika kuadhimisha sikuku ya Eid Elhaji, Polisi Mkoa wa Magharibi walifanya operesheni mbalimbali na katika operesheni hizo wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 37 kwa makosa mbali mbali ya kiuhalifu.