“Kila Rais alieingia madarakani aliperfom vizuri sana kwa namna yake lakini namna hizi zao kama kila Mtu ana namna yake unategemea Nchi itaendeleaje kwasababu kila Mtu ana namna yake na namna ya mmoja ni kinyume ya namna ya aliyetoka tutaendaje? hii inanipelekea kusema Ili tuendelee tunahitaji ajenda ya pamoja ya Taifa lote kwa namna gani sasa” Gwajima
“Tudefine maono ya Tanzania ya miaka 30 au 50, tuwe na vitu ambavyo sisi Watanzania tutaviita maendeleo sio lazima vitu hivyo viitwe maendeleo Marekani kwa mfano ujenzi wa maghorofa si maendeleo kwetu, tunaweza kusema maendeleo kwetu kila Mtanzania awe na maji salama na safi” Gwajima
“Tunaweza kusema maendeleo kwetu kila Mtanzania mwenye uwezo wa kusoma shule asome Chuo Kikuu na amalize asiwepo wa kutokusoma Chuo Kikuu, tunaweza kusema maendeleo kwetu sisi Wafanyabiashara wafanye biashara vizuri tuwe tunaexport”———Askofu Josephat Gwajima, Mbunge wa Jimbo la Kawe
“Tusipofanya hivi tuna hatari kwasababu katiba yetu inampa nafasi kila Rais anayeingia madarakani kwa namna yake kwa hekma yake na kwa namna anavyotafsiri yeye maendeleo na siku moja tutakapopata Rais ambaye hayuko sawasawa tutaishia kulia” Gwajima
“Ni ombi langu tuwe na maono ya miaka 50 halafu anapoingia Rais lazima ilani ya Chama chake izungumze mambo ambayo sisi tumejiwekea kama maono ya Tanzania mfano patakapotokea Rais akaanza kufanya mambo yake kuna Mtu wa kumuuliza hapa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Amiri Jeshi Mkuu kwamba hutakiwi kufanya haya lakini tutakapokuwa na vision ambayo imewekwa kwamba tunahitaji kufikia mambo kadhaa wa kadhaa na kila regime inapoingia iwe ya kijani au blue utatimiza yale ambayo sisi tumejiwekea kama maendeleo kwetu na maono ya Taifa letu”——— Josephat Gwajima